2 Mambo ya Nyakati UTANGULIZI - Swahili Revised Union Version

UTANGULIZIKitabu hiki kinaendeleza masimulizi ya Kitabu cha Kwanza, kikianzia pale cha Kwanza kilipomalizika. Mwandishi anaanza na habari za Solomoni na jambo kubwa kwake ni ujenzi wa hekalu. Ufalme wa Kaskazini haushughulikiwi kwa kuwa uongozi wake hautokani na nasaba ya Daudi. Mtawala anayesifiwa ni yule aliyetokana na nasaba ya Daudi, akafuata mafundisho ya makuhani wa Kilawi. Mwandishi anaeleza kwa kirefu shughuli za matengenezo ya kidini hali shughuli za kisiasa zinaelezwa kwa kifupi.Mwandishi anasimulia mitafaruku kati ya makabila ya Kaskazini na Kusini. Sehemu kubwa anaeleza Ufalme wa Kusini hadi mji wa Yerusalemu ulipoangamizwa. Mwandishi ana mkazo maalumu kuhusu taifa na dini. Heri ya Israeli ilitokana na Mungu: aidha ahadi za Mungu kwa Daudi zilitimilika, ikiwa watu walikuwa waaminifu kwa Agano, na kufuata mapenzi ya Mungu.Yaliyomo:1. Utawala wa mfalme Sulemani, Sura 1—8(a) Kufaulu kwa Sulemani, (1)(b) Kujenga hekalu na sanduku la Agano kuletwa hekaluni (2—7)(c) Utukufu wa Sulemani (8—9)2. Kugawanywa kwa Israeli, Sura 103. Wafalme wa Kusini inayoitwa Yuda, Sura 11:1—36:144. Kuangamizwa kwa Yerusalemu, Sura 36:15-215. Tangazo la Koreshi: Wayahudi kurudi na kujenga hekalu, Sura 36:22-23
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help