Marko 9 - Swahili Revised Union Version

Kugeuka sura

1Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.

2 Yesu asema juu ya kufa na kufufuka kwake tena

30 Mt 17:22,23; Lk 9:43-45 Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua.Yn 7:1

31Mk 8:31; 10:32-34 Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; na akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka.

32Lk 9:45; 18:34 Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.

Ni nani mkubwa wa wote

33 Mt 18:1-9; Lk 9:46-50 Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani?Mt 17:24

34Lk 22:24 Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.

35Mt 20:26-27; 23:11; Mk 10:43-44; Lk 22:26 Akaketi chini, akawaita wale Kumi na Wawili akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.

36Mk 10:16 Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia,

37Mt 10:40; Lk 10:16; Yn 13:20 Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

Mtoa Pepo Mwingine

38 Hes 11:27,28 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi.

391 Kor 12:3 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu na punde baadaye akaweza kuninena kwa uovu;

40Mt 12:30; Lk 11:23 kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.

41Mt 10:42 Kwa kuwa yeyote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.

Majaribu ya dhambi

42Na yeyote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini.

43Mt 5:30 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kibutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako Jehanamu, kwenye moto usiozimika;

45Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, ukiwa kiguru, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika Jehanamu;

47Mt 5:29 Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika Jehanamu;

48Isa 66:24 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

49Law 2:13 Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.

50Mt 5:13; Lk 14:34-35; Kol 4:6 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help