1Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang'anyi.
2Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
3Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.
4Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake.
5Yn 10:27 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.
6Yn 16:25 Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa mambo hayo aliyowaambia.
7 Zab 118:20; Yn 14:6; Mt 7:13,14 Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.
8Yer 23:1,2 Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.
9Zab 118:20; Yn 14:6; 1 Kor 3:15 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
10Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.
11Zab 23:1; Lk 15:4-7 Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
12Isa 40:11; Eze 34:11-23; 37:24; Yn 15:13; Mt 10:16; Mdo 20:29; Tit 1:11; 1 Pet 5:2,3 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
13Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake.
142 Tim 2:19 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
15Mt 11:27; Lk 10:22 kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
16Eze 37:24; 34:23; Yn 11:52; 1 Pet 2:25; Efe 4:5 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
17Flp 2:8,9 Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena.
18Yn 5:26; 19:11 Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nililipokea kwa Baba yangu.
19 Yn 7:43; 9:16 Kukawa na utengano tena kati ya Wayahudi, kwa ajili ya maneno hayo.
20Yn 7:20; 8:48; Mk 3:21 Wengi wao wakasema, Ana pepo huyu, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?
21Wengine wakasema, Maneno hayo siyo ya mtu mwenye pepo. Je! Pepo aweza kuwafumbua macho vipofu?
Yesu akataliwa na Wayahudi22Basi huko Yerusalemu ilikuwa sikukuu ya kutabaruku; ni wakati wa baridi.
23Mdo 3:11; 5:12 Naye Yesu alikuwa akitembea hekaluni, katika ukumbi wa Sulemani.
24Lk 22:67 Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
25Yn 4:26; 5:36; 9:37 Yesu akawajibu, Niliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia.
26Yn 6:64; 8:45 Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wangu.
27Yn 8:47; 10:3,4 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
28Yn 5:28; 6:39; 17:12; 18:9 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
29Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
30Mimi na Baba tu mmoja.
31Yn 8:59 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.
32Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?
33Law 24:16; Yn 5:18; Mt 26:65 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.
34Zab 82:6 Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?
35Mt 5:17,18 Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
36Yn 5:17-20 je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nilisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
37Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini;
38lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba.
39Yn 8:59; Lk 4:30 Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao.
40 Yn 1:28 Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko.
41Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini yote aliyoyasema Yohana kuhusu habari zake huyu yalikuwa kweli.
42Yn 8:30 Nao wengi wakamwamini huko.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.