Ezekieli 47 - Swahili Revised Union Version

Maji yatokayo hekaluni

1 maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yatakuwa safi.

9Yn 5:25; 6:63; 1 Kor 15:45 Tena itakuwa, kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; kutakuwapo wingi mkubwa wa samaki, kwa sababu maji haya yamefika huko maana maji yale yatakuwa safi, na kila kitu kitaishi popote utakapofika mto huo.

10Mt 4:19; Hes 34:6; Yos 23:4; Eze 47:15 Tena itakuwa, wavuvi watasimama karibu nao; toka Engedi mpaka En-eglaimu, patakuwa ni mahali pa kutandazia nyavu; samaki wao watakuwa namna zao mbalimbali, kama samaki wa bahari kubwa, wengi sana.

11Bali mahali penye matope, na maziwa yake, hayataponywa; yataachwa yawe ya chumvi.

12Ayu 8:16; Zab 1:3; Isa 61:3; Ufu 22:2 Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.

Mipaka mipya ya nchi

13 Mwa 48:5; 1 Nya 5:1; Yer 3:18; Eze 48:4,5 Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio mpaka ambao mtaigawanya nchi iwe urithi sawasawa na makabila kumi na mawili ya Israeli; kwa Yusufu, mafungu mawili.

14Hes 34:2; Eze 48:29 Nanyi mtaimiliki, mtu huyu sawasawa na huyu; ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa baba zenu; na nchi hii itawaangukia kuwa urithi.

15Eze 48:1; Hes 34:8 Na huu ndio mpaka wa nchi; upande wa kaskazini, toka bahari kubwa, kwa njia ya Hethloni, mpaka maingilio ya Sedada;

162 Fal 14:25; Amo 6:2,14; 2 Sam 8:8 Hamathi, na Berotha, na Sibraimu, ulio katikati ya mpaka wa Dameski na mpaka wa Hamathi; na Haser-hatikoni, ulio karibu na mpaka wa Haurani.

17Hes 34:9 Nao mpaka toka baharini utakuwa Hasar-enoni, penye mpaka wa Dameski, na kaskazini kuelekea upande wa kaskazini ndio mpaka wa Hamathi. Huu ndio upande wa kaskazini.

18Na upande wa mashariki, kati ya Haurani na Dameski, na Gileadi na nchi ya Israeli, utakuwa Mto Yordani; mtapima toka mpaka wa upande wa kaskazini hata bahari ya mashariki. Huu ndio upande wa mashariki.

19Na upande wa kusini, kuelekea kusini, utakuwa ni kutoka Tamari mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. Huu ndio upande wa kusini, kuelekea kusini.

20Na upande wa magharibi, utakuwa ni bahari kubwa, kutoka mpaka wa kusini mpaka mahali penye kuelekea maingilio ya Hamathi. Huu ndio upande wa magharibi.

21Basi ndivyo mtakavyojigawanyia nafsi zenu nchi hii, sawasawa na makabila ya Israeli.

22Mdo 2:5; Efe 2:19-22; Rum 10:12 Tena itakuwa mtaigawanya kwa kura, kuwa urithi kwenu, na kwa wageni wakaao kwenu kama ugeni, watakaozaa watoto kati yenu, nao watakuwa kwenu, kama wazaliwa miongoni mwa wana wa Israeli; watakuwa na urithi pamoja nanyi kati ya makabila ya Israeli.

23Tena itakuwa, mgeni akaaye katika kabila iwayo yote, atapewa urithi katika kabila asema Bwana MUNGU.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help