1 ndiyo Hebroni (ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki).
14Amu 1:10; Hes 13:22 Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wazawa wa Anaki.
15Yos 10:38 Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.
16Kalebu akasema, Yeyote atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe.
17Amu 3:9; Hes 32:12; Yos 14:6 Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe.
18Amu 1:14; Mwa 24:64; 1 Sam 25:23 Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini?
19Mwa 33:11 Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya upande wa juu, na chemchemi za maji yaupande wa chini.
Miji ya Yuda20 Mwa 49:8-12; Kum 33:7 Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.
21 Mwa 35:21 Miji ya mwisho ya kabila la wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, Ederi, Yaguri;
22Kina, Dimona, Adada;
23Kedeshi, Hazori, Ithnani;
241 Sam 15:4 Zifu, Telemu, Bealothi;
25Hazor-hadata, Kerioth-hezroni (ndio Hazori);
26Amamu, Shema, Molada;
27Hasar-gada, Heshmoni, Beth-peleti;
28Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia;
29Baala, Iyimu, Esemu;
30Eltoladi, Kesili, Horma;
31Yos 19:5; 1 Sam 27:6; 30:1; 1 Nya 12:1 Siklagi, Madmana, Sansana;
32Neh 11:29 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.
33 Yos 19:41; Hes 13:23 Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, Sora, Ashna,
34Zanoa, Enganimu, Tapua, Enamu;
35Yos 10:3,5; 12:15; 1 Sam 17:1; Yos 10:10 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka;
361 Sam 17:52 Shaarimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.
37Senani, Hadasha, Migdal-gadi;
382 Fal 14:7 Dilani, Mispe, Yoktheeli;
39Yos 10:3; 2 Fal 18:14; 19:8; 2 Nya 11:9; 2 Fal 22:1; Yos 12:12 Lakishi, Bozkathi, Egloni;
40Kaboni, Lamasi, Kithilishi;
41Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
42Libna, Etheri, Ashani;
43Yifta, Ashna, Nesibu;
44Keila, Akizibu na Maresha; miji tisa, pamoja na vijiji vyake.
45Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake;
46Yos 13:3; 1 Sam 5:1,6 kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake.
47 Mwa 15:18; Hes 34:6 Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake.
48Na katika nchi ya vilima, Shamiri, Yatiri, Soko;
49Dana, Kiriath-sana (ambao ni Debiri);
50Anabu, Eshtemoa, Animu;
51Yos 10:41; 11:16 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.
52Arabu, Duma, Eshani;
53Yanumu, Beth-tapua, Afeka;
54Mwa 23:2; Yos 14:15; Amu 1:10 Humta, Kiriath-arba (ndio Hebroni) na Siori; miji tisa, pamoja na vijiji vyake.
55Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta;
56Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa;
57Kaini, Gibea na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.
58Halhuli, Beth-suri, Gedori;
59Maarathi, Bethanothi na Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60 Yos 18:14; 1 Sam 7:1,2; 1 Nya 13:6 Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu) na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.
61Huko nyikani, Beth-araba, na Midini, na Sekaka;
621 Sam 23:29 na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
63 Amu 1:8,21; 19:10-12; Hes 13:29; 2 Sam 5:6; 24:16,18; 1 Nya 11:4; 2 Nya 3:1; Zek 9:7 Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.