1 Mambo ya Nyakati 7 - Swahili Revised Union Version

Wazawa wa Isakari

1 Mwa 30:17,18; 46:13; Hes 26:23 Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne.

22 Sam 24:1,2; 1 Nya 21:1-5; 27:1 Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa koo za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita.

31 Nya 5:24 Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu.

4Na pamoja nao, katika vizazi vyao, kulingana na koo za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu elfu thelathini na sita; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi.

5Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu elfu themanini na saba.

Wazawa wa Benyamini

6 Mwa 46:21; Hes 26:38; 1 Nya 8:1 Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu.

7Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne.

8Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri.

9Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu elfu ishirini na mia mbili.

10Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari.

11Hao wote ndio wana wa Yediaeli, kulingana na wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, elfu kumi na saba na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.

12Hes 26:38,39 Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.

Wazawa wa Naftali

13 Mwa 46:24 Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shalumu; wana wa Bilha.

Wazawa wa Manase

14 Hes 27:1 Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;

15Hes 27:1-11 naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao dada yao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.

16Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.

171 Sam 12:11 Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.

18Na dada yake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.

19Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.

Wazawa wa Efraimu

20 Mwa 41:52; 48:14-20; Hes 26:35,36; Kum 33:13,17; Zab 60:7; 108:8 Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;

21na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuwapokonya ng'ombe wao.

22Mwa 37:34,35; Yos 7:6; 2 Sam 1:11; 3:31; Ayu 2:11; Zab 69:11; Yoe 2:13; Yn 11:19 Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji.

23Mwa 35:18; 1 Sam 4:21; 1 Nya 4:9 Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu maafa yalikuwa yameipata nyumba yake.

24Yos 16:3; 1 Sam 13:18; 2 Nya 8:5 Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.

25Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani;

26na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama;

27Hes 13:8,16 na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.

28Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;

29Yos 17:7,11; 1 Fal 9:15; Amu 1:22-29 na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.

Wazawa wa Asheri

30 Mwa 46:17; 49:20; Hes 26:44,46; Kum 33:24 Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na dada yao, Sera.

31Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.

32Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na dada yao, Shua.

33Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti.

34Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.

35Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali.

36Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra;

37na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera.

38Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara.

39Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia.

40Kum 2:14 Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa koo za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, viongozi wa wakuu. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu elfu ishirini na sita.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help