Ruthu 3 - Swahili Revised Union Version

Ruthu na Boazi kwenye uga wa kupepetea

1 1 Kor 7:36; 1 Tim 5:8; Kum 4:40; Rut 1:9; Zab 128:2; Yer 22:15,16 Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema?

2Rut 2:8 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani.

32 Sam 14:2 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; lakini usijioneshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa.

4Nayo itakuwa wakati atakapolala, utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na yeye atakuambia utakalofanya.

5Efe 6:1; Kol 3:20 Akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya.

6Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza.

7Amu 19:6; 2 Sam 13:28; Est 1:10 Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa rundo la nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo.

8Na ikawa usiku wa manane yule mtu akashtuka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake.

9Eze 16:8 Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu.

10Rut 2:20; 1:8 Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.

11Mit 12:4; 31:10,29,31 Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.

12Rut 2:20; 4:1; 1 The 4:6 Tena ni kweli kuwa mimi ni jamaa yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi.

13Kum 25:5; Rut 4:5; Mt 22:24; Amu 8:19; Yer 4:2; Ebr 6:16 Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hadi asubuhi.

14Rum 12:17; 14:16; 1 Kor 10:32; 2 Kor 8:21; 1 The 5:22; 1 Pet 2:12 Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe; maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga.

15Tena alisema, Lete hapa shela yako uliyoivaa, uishike; naye akaishika; naye akampimia vipimo sita vya shayiri akamtwika; kisha huyo mwanamke akaenda zake mjini.

16Basi alipofika kwa mkwewe, huyo akamwuliza, Je! Mwanangu, imekuwaje? Akamwambia yote yule mtu aliyomfanyia.

17Akasema, Na vipimo hivi sita vya shayiri amenipa; maana aliniambia, Usiende kwa mkweo mikono mitupu.

18Naye mkwewe akasema, Basi, mwanangu, tulia; hadi utakapojua jinsi litakavyotukia jambo hili; kwa sababu mtu huyu hataridhika, asipolimaliza jambo hilo leo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help