Isaya 55 - Swahili Revised Union Version

Mwaliko wa maisha mema

1 Yn 4:14; 7:37; 1 Kor 1:22; Mt 13:44; Ufu 21:6; 3:18; 22:17 Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,

Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;

Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,

Bila fedha na bila gharama.

2Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?

Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?

Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,

Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

3 Mt 11:28; Isa 54:8; 2 Sam 7:8; Zab 89:28; Mdo 13:34 Tegeni masikio yenu, na kunijia;

Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;

Nami nitafanya nanyi agano la milele,

Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

4 Mal 3:5; 1 Tim 6:13; Ufu 1:5; Eze 34:23; Dan 9:25; Ebr 2:10 Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu.

5Isa 52:15; Efe 2:11,12; Mdo 3:13 Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

6 Zab 32:6; Amo 5:4,14; Mt 5:25; Yn 7:34; 2 Kor 6:2; Ebr 3:13 Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,

Mwiteni, maadamu yuko karibu;

7 Zek 8:17; Yer 3:12 Mtu mbaya na aache njia yake,

Na mtu asiye haki aache mawazo yake;

Na amrudie BWANA,

Naye atamrehemu;

Na arejee kwa Mungu wetu,

Naye atamsamehe kabisa.

8Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.

9Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

102 Kor 9:10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;

11ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

12Maana mtatoka kwa furaha,

Mtaongozwa kwa amani;

Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;

Na miti yote ya shambani itapiga makofi.

13Badala ya michongoma utamea msonobari,

Na badala ya mibigili, mhadesi;

Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina,

Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help