Marko 16 - Swahili Revised Union Version

Kufufuka kwa Yesu

1 Mt 28:1-8; Lk 24:1-12; Yn 20:1-10 Na sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

2Na alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;

3wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?

4Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno.

5Wakaingia kaburini wakaona kijana akiwa ameketi upande wa kulia, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu.

6Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka.

7Mt 26:32; Mk 14:28 Lakini nendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia.

8Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingiwa na hofu na mshangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.

Yesu amtokea Mariamu Magdalene

[

9Lk 8:2; Yn 20:11-18 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye alikuwa amemtoa pepo saba.

10Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wapokuwa wanaomboleza na kulia.

11Lakini hao waliposikia kwamba yu hai, naye amemwona, hawakuamini.

Yesu awatokea wanafunzi wawili

12 Lk 24:13-35 Baada ya hayo akawatokea wawili miongoni mwao, akiwa na sura nyingine; nao walikuwa wakitembea njiani kwenda mashambani.

13Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwaamini.

Yesu awatuma wanafunzi

14 Lk 24:36-49; Yn 20:19-23 Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.

15Mdo 1:8; Mt 28:18-20 Akawaambia, Nendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16Mdo 2:38 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

17Mdo 16:18; 2:4,11; 10:46 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

18Lk 10:19; Mdo 28:3-6; Yak 5:14,15 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.

Kupaa kwa Yesu

19 Mdo 1:9-11; Lk 24:50-53; 1 Tim 3:16; Zab 110:1; Mdo 7:55; 2 Fal 2:11 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kulia wa Mungu.

20Ebr 2:4 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help