Matendo 8 - Swahili Revised Union Version

Sauli alitesa kanisa

1 Mdo 7:58; 11:19; 22:20 Siku ile kukatokea mateso makuu kwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Yudea na Samaria, isipokuwa hao mitume.

2Mt 14:12 Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.

3Mdo 22:4-5; 9:1; 26:9-11 Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.

Filipo ahubiri katika Samaria

4Lakini wale waliotawanyika wakaenda huku na huko wakilihubiri neno.

5Mdo 6:5 Filipo akateremka akaingia katika mji wa Samaria, akawahubiria Kristo.

6Na mkutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya.

7Mk 16:17 Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa.

8Yn 4:40-42 Ikawa furaha kubwa katika mji ule.

9Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.

10Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, aliye Mkuu.

11Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.

12Mt 28:19 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

13Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka.

14 Mdo 3:1 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;

15ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;

16kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.

171 Tim 4:14 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.

18Wakati Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,

19Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.

20Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.

21Zab 78:37; Efe 5:5 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.

22Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili ikiwezekana, usamehewe fikira hii ya moyo wako.

23Kum 29:18; Isa 58:6; Ebr 12:15 Kwa maana nakuona uko katika uchungu kama nyongo, na tena uko katika kifungo cha uovu.

24Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikie mambo haya mliyosema hata moja.

25Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.

Filipo na towashi wa Ethiopia

26Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile iteremkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.

27 Isa 56:3-7 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyesimamia hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu,

28akawa akirudi nyumbani, akiwa ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya.

29Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukaribiane nalo.

30Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma kitabu cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?

31Yn 16:13 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.

32Isa 53:7-8 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili,

Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo,

Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya,

Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

33Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa.

Ni nani atakayeeleza kizazi chake?

Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.

34Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?

35Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiria Habari Njema za Yesu.

36Mdo 10:47 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

38Akaamuru lile gari lisimame; wakateremka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.

391 Fal 18:12 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.

40Mdo 21:8,9 Lakini Filipo akaonekana katika Azota, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hadi akafika Kaisaria.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help