1Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na kuabiri, tukafika Kosi kwa tanga moja, na kesho yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,
2tukapata merikebu itakayovuka mpaka Foinike tukapanda tukatweka.
3Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.
4Mdo 11:12; 20:23 Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paulo kwa uweza wa Roho asipande kwenda Yerusalemu.
5Mdo 20:36 Hata tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote, pamoja na wake zao na watoto wao, wakatusindikiza mpake nje ya mji, tukapiga magoti pwani tukaomba;
6na baada ya kuagana tukapanda melini, nao wakarudi kwao.
7Tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai, tukawaamkua ndugu tukakaa kwao siku moja.
8Mdo 6:5; 8:5,40 Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.
9 Mdo 2:17 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri.
10Mdo 11:28 Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Yudea.
11Mdo 20:23 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.
12Mt 16:22 Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.
13Mdo 20:24 Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.
14Mt 26:39; Yn 21:18 Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke.
15Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemu.
16Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakamchukua na Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani ambaye ndiye tutakayekaa kwake.
Paulo amtembelea Yakobo Yerusalemu17Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha.
18Mdo 15:13; Gal 1:19 Hata kesho yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako.
19Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake.
20Mdo 15:1 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.
21Mdo 16:3; Rum 10:4 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi.
22Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja.
23Hes 6:13-21 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri.
24Mdo 18:18 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.
25Mdo 15:20,29 Lakini kuhusu watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.
26Hes 6:1-20; 1 Kor 9:20 Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na kesho yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao.
Paulo ashikwa akiwa hekaluni27Basi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimia, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata,
28Mdo 6:13; Eze 44:7 wakapiga kelele, na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wagiriki katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu.
29Mdo 20:4; 2 Tim 4:20 Kwa maana walikuwa wamemwona Trofimo, Mwefeso, pamoja naye mjini, ambaye walidhania ya kuwa Paulo amemwingiza katika hekalu.
30Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni; mara milango ikafungwa.
31Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, habari zikamfikia jemadari wa kikosi ya kwamba Yerusalemu imechafuka, mji mzima.
32Mara akatwaa askari na maofisa, akawaendea mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.
33Mdo 21:11; 20:23 Kisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili; akauliza, Nani huyu? Tena, amefanya nini?
34Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.
35Basi Paulo alipofika darajani ilikuwa kuchukuliwa na askari kwa sababu ya nguvu ya makutano.
36Mdo 22:22; Lk 23:18 Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, na kusema, Na aondolewe mbali.
Paulo ajitetea37Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kigiriki?
38Mdo 5:36,37 Wewe si yule Mmisri ambaye kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani?
39Mdo 9:11 Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.
40Basi, alipompa ruhusa, Paulo akasimama madarajani, akawapungia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.