1 Mambo ya Nyakati 21 - Swahili Revised Union Version

Hesabu na tauni

1 Myebusi.

162 Nya 3:1 Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa BWANA amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusalemu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifudifudi, nao wamevaa nguo za magunia.

17Daudi akamwambia Mungu, Je! Si mimi niliyeamuru watu wahesabiwe? Naam, mimi ndimi niliyekosa, na kufanya yaliyo maovu sana; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako, nakusihi, Ee BWANA, Mungu wangu, na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya babangu; wala si juu ya watu wako, hata wao wapigwe.

Madhabahu ya Daudi na sadaka yake

18Ndipo huyo malaika wa BWANA akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie BWANA madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.

19Basi Daudi akakwea kulingana na neno la Gadi, alilolinena kwa jina la BWANA.

20Arauna alipogeuka, na kumwona yule malaika, ndipo yeye na wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha. Naye Arauna alikuwa akipura ngano.

21Basi Daudi alipokuwa akimjia Arauna, Arauna akatazama, akamwona Daudi, akatoka katika kile kiwanja, akamsujudia Daudi kifudifudi hadi chini.

22Hes 16:48; 25:8 Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja hiki, ili kwamba nimjengee BWANA madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili kwamba tauni izuiliwe katika watu.

23Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa.

24Mfalme Daudi akamwambia Arauna, La, sivyo, lakini kweli nitazinunua kwa thamani yake kamili; kwani sitamtwalia BWANA kilicho chako, wala kutoa sadaka ya kuteketezwa isiyo na gharama.

252 Sam 24:24 Basi Daudi akampimia Arauna thamani ya mahali pale shekeli mia sita za dhahabu kwa uzani

26Law 9:24; 2 Nya 3:1; 7:1 Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.

27BWANA naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena.

Mahali pa kujenga hekalu pachaguliwa

28Wakati huo, Daudi alipoona ya kwamba BWANA amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo alipotoa dhabihu huko.

291 Nya 16:39; 1 Fal 3:4; 2 Nya 1:3 Kwa maana ile maskani ya BWANA, aliyoifanya Musa jangwani, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, vilikuwapo wakati huo mahali pa juu pa Gibeoni.

302 Sam 6:9; 1 Nya 13:12; Ayu 13:21; 21:6; Zab 119:120 Wala Daudi hakuweza kwenda mbele yake ili kumwuliza Mungu; kwa sababu aliona hofu kwa ajili ya upanga wa yule malaika wa BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help