1 nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
19Yak 2:10; 1 Kor 15:9 Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Kuhusu hasira21 Kut 20:13; 21:12; Law 24:17; Kum 5:17; 17:8 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
221 Yoh 3:15 Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
23Mk 11:25 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
25Mt 6:14,15; 18:35; Lk 12:58,59 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho.
Kuhusu uzinzi27 Kut 20:14; Kum 5:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28Ayu 31:1; 2 Pet 2:14 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29Mt 18:8,9; Mk 9:42,47; Kol 3:5 Jicho lako la kulia likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote utupwe katika Jehanamu.
30Mt 18:8; Mk 9:43 Na mkono wako wa kulia ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote kutupwa katika Jehanamu.
Kuhusu talaka31 Kum 24:1-4; Mt 19:7; Mk 10:4 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18; 1 Kor 7:10-11 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Kuhusu viapo33 Law 19:12; Hes 30:2; Kum 23:21; Kut 20:7 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;
34Yak 5:12; Isa 66:1; Mt 23:16-22; Mdo 7:49 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35Isa 66:1; Zab 48:2 wala kwa nchi, kwa maana ndipo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
372 Kor 1:17; Yak 5:12 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Kuhusu kujilipiza kisasi38 Kut 21:24; Law 24:20; Kum 19:21 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39Lk 6:27-36 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili. Yn 18:22,23; Law 19:18
401 Kor 6:7 Na mtu atakaye kukushitaki na kulichukua shati lako, mwachie na koti pia.
41Mtu yeyote akikulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye maili mbili.
42Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
Upendo kwa adui43 Law 19:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44Kut 23:4,5; Rum 12:14,20; Lk 23:34; Mdo 7:59 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45Efe 5:1 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mnapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo?
48Law 19:2; Kum 18:13 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.