1 Kum 16:18; Amu 10:4; 12:14 Na Samweli alipozeeka, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.
2Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza lilikuwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.
3Mhu 2:19; Yer 22:15; Kut 18:21; Kum 16:19; 1 Tim 3:3; 6:10; Zab 15:5 Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu.
4Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
5Kum 17:14; 1 Sam 12:13; Hos 13:10; Mdo 13:21 wakamwambia, Angalia, wewe umezeeka, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tuteulie mfalme atutawale kama mataifa yale mengine yote.
6Kut 32:31,32; 1 Sam 15:11; Mit 3:5 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA.
7Kut 16:8; Mt 10:24,25; Lk 10:16; Yn 13:16; 1 Sam 10:19 BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
8Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.
9Basi sasa, isikilize sauti yao; lakini, uwaonye sana, na kuwaonesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.
10Naye Samweli akawaambia wale watu waliotaka mfalme maneno yote ya BWANA.
11Kum 17:16; 1 Sam 10:25; 14:52; 2 Nya 26:10-15 Akasema, Mfalme atakayewatawala ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, katika magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.
12Naye atawaweka kwake kuwa wakuu juu ya maelfu, na makamanda juu ya hamsini hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.
13Na binti zenu atawatwaa kuwa watengenezaji wa marhamu, wapishi na waokaji.
141 Fal 21:7 Atatwaa mashamba yenu, na mashamba yenu ya mizabibu, na ya mizeituni, yale yaliyo mazuri sana, ili awape watumishi wake.
15Naye atawatoza ushuru wa mbegu zenu na wa mizabibu yenu, awape wakuu wake, na watumishi wake.
16Atawatwaa watumishi wenu na wajakazi wenu, na ng'ombe wenu walio wazuri sana, na punda wenu, naye atawatia katika kazi zake mwenyewe.
17Atawatoza fungu la kumi la mifugo wenu; nanyi mtakuwa watumwa wake.
18Ayu 27:9; Zab 18:41; Mit 1:25; Isa 1:15; Mik 3:4; Lk 13:25 Nanyi mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyejichagulia; BWANA asiwajibu siku ile.
Waisraeli wapewa mfalme19 Isa 66:4; Yer 44:16 Lakini hao watu wakakataa kuisikiliza sauti ya Samweli; wakasema, Sivyo hivyo; lakini tunataka kuwa na mfalme juu yetu;
20ili sisi nasi tufanane na mataifa yote; tena ili mfalme wetu atuamue, tena atuongoze na kupigana vita vyetu
21Samweli akayasikia maneno yote ya watu, akayanena masikioni mwa BWANA.
22Hos 13:11 BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti yao, ukawateulie mfalme. Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, Kila mtu aende nyumbani kwake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.