1 mwingi kwa wote wamwitao;
13Yoe 2:32 kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
14Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
15Isa 52:7 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
16 Isa 43:1 Lakini si wote walioitii ile Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu?
17Yn 17:20 Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
18Zab 19:4 Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia,
Sauti yao imeenea duniani kote,
Na maneno yao hadi katika miisho ya ulimwengu.
19 Kum 32:21 Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena,
Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa,
Kwa taifa lisilo na fahamu nitawakasirisha.
20 Isa 65:1 Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema,
Nilipatikana nao wasionitafuta,
Nilidhihirika kwao wasioniulizia.
21 Isa 65:2 Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.