Marko 3 - Swahili Revised Union Version

Mtu mwenye mkono uliopooza

1 Mt 12:9-14; Lk 6:6-11 Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;

2wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.

3Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.

4Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.

5Yn 11:33 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.

6Mt 22:16 Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza.

Watu wengi kando ya ziwa

7 Mt 12:15,16; Lk 6:17-19 Naye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Yudea,

8Mt 4:25 na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.

9Mk 4:1; Lk 5:1-3 Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba mashua ndogo ikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.

10Maana aliponya wengi, hata wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa.

11Lk 4:41 Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.

12Mk 1:34 Akawakataza sana, wasimdhihirishe.

Yesu awateua wale kumi na wawili

13 Mt 10:1-4; Lk 6:12-16 Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea.

14Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri,

15tena wawe na mamlaka ya kutoa pepo.

16Yn 1:42 Akawaweka wale Kumi na Wawili; na Simoni akampa jina la Petro;

17Lk 9:54 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;

18na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,

19na Yuda Iskarioti, ndiye aliyemsaliti.

Yesu na Belzebuli

Kisha akaingia nyumbani.

20Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate.

21Yn 7:20; 8:48,52; 10:20 Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.

22Mt 12:24-32; Lk 11:15-22; 12:10 Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.Mt 9:34; 10:25

23Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?

24Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;

25na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.

26Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.

27Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

28Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;

29Lk 12:10 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,

30Mk 3:22 kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.

Jamaa wa kweli wa Yesu

31 Mt 12:46-50; Lk 8:19-21 Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita.

32Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.

33Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?

34Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu!

35Kwa maana mtu yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help