1 mnaoapa kwa jina la BWANA, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki.
2Mik 3:11; Rum 2:17 Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; BWANA wa majeshi ni jina lake.
3Yos 21:45 Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; niliyatenda kwa ghafla, yakatokea.
4Kut 32:9; Kum 31:27 Kwa sababu nilijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba;
5basi nimekuonesha tangu zamani; kabla hayajatukia nilikuonesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru.
6Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua.
7Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, niliyajua.
8Zab 58:3 Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
9Yos 7:9; Zab 106:8 kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali.
10Zab 66:10; Isa 1:25; Mal 3:3 Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso.
11Kum 32:26; Isa 42:8 Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.
12 Kum 32:39; Isa 44:6; Ufu 1:17; 22:13 Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.
13Zab 102:25 Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kulia umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja.
14Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.
15Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake.
16Zek 2:8,9 Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.
17Zab 32:8 BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
18Kum 5:29; Zab 81:13 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
19Mwa 22:17; Hos 1:10 Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.
20 Zek 2:6,7; Kut 19:4; Ufu 18:4 Haya, tokeni katika Babeli,
Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo;
Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya,
Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni,
BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.
21 Hes 20:11; Neh 9:15; Zab 105:41; Isa 48:21; 1 Kor 10:4 Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani;
Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao;
Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.
22 Isa 57:21 Hapana amani kwa waovu, asema BWANA.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.