1 Rum 6:11,13; 1 Pet 2:5; Yn 4:24 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2Efe 4:23; 5:10,17; Rum 1:28; Gal 1:4 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
3 1 Kor 12:11; Efe 4:7 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
41 Kor 12:12 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;
51 Kor 12:27; Efe 4:25 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
61 Kor 12:4-11 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa ni unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
71 Pet 4:10,11 ikiwa ni huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8Mt 6:3; 2 Kor 8:2; 9:7 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; msimamizi, na asimamie kwa bidii; anayerehemu, na arehemu kwa furaha.
Sifa za Mkristo9 1 Pet 1:22; 1 Tim 1:5; Amo 5:15 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkilishika lililo jema.
102 Pet 1:7; Flp 2:3 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11Ufu 3:15; Mdo 18:25 kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
121 The 5:17 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;
13Ebr 13:2 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
14Mt 5:44; Lk 6:28; Mdo 7:59; 1 Kor 4:12 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
15Zab 35:13 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
16Mit 3:7; Rum 15:5; 11:20 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
17Isa 5:21; 1 The 5:15 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18Mk 9:50; Ebr 12:14 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19Kum 32:35; Law 19:18; Mt 5:39; 2 The 1:6,7; Rum 13:4; Ebr 10:30 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20Mit 25:21-22; Mt 5:44 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.