Warumi 15 - Swahili Revised Union Version

Pendezeni wengine wala sio kujipendeza wenyewe

1Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.

21 Kor 9:19; 10:24,33 Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.

3Zab 69:9 Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Matusi yao waliokutusi wewe yalinipata mimi.

4Rum 4:23,24; 1 Kor 10:11 Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.

5Flp 3:16 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunuia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa kufuata mfano wa Kristo Yesu;

6ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Injili kwa Wayahudi na Wamataifa

7Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.

8Mt 15:24; Mdo 3:25 Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;

92 Sam 22:50; Zab 18:49; Rum 11:30 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa,

Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa,

Nami nitaliimbia jina lako.

10 Kum 32:43 Na tena anena,

Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.

11 Zab 117:1 Na tena,

Enyi Mataifa yote, msifuni Bwana;

Enyi watu wote, mhimidini.

12 Isa 11:10; Ufu 5:5 Na tena Isaya anena,

Litakuwako shina la Yese,

Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;

Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

13Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Sababu ya Paulo kuandika kwa ujasiri

14Ndugu zangu, mimi mwenyewe nina hakika juu yenu, kuwa ninyi mmejaa wema, na mmejazwa ujuzi wote, tena mnaweza kuonyana.

15Rum 1:5; 12:3 Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu,

16Rum 11:13; Flp 2:17 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.

17Basi, nina sababu ya kuona fahari katika Kristo Yesu mbele za Mungu.

182 Kor 3:5 Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo,

19Mk 16:17 kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kandokando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu;

202 Kor 10:15,16 kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine;

21Isa 52:15 bali kama ilivyoandikwa,

Wale wasiowahi kuhubiriwa habari zake wataona,

Na wale wasiowahi kusikia habari zake watafahamu.

Mpango wa Paulo kuutembelea Rumi

22 Rum 1:10-13 Ndiyo sababu nilizuiwa mara nyingi nisije kwenu.

23Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena kwa miaka mingi nimekuwa nikitamani kuja kwenu;

241 Kor 16:6 wakati wowote nitakaosafiri kwenda Spania Kwa maana natarajia kuwaona ninyi nikiwa katika safari, na kusafirishwa nanyi, baada ya kukaa kwenu kwa muda.

251 Kor 16:1-4 Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumia watakatifu; Mdo 19:21; 20:22

261 Kor 16:1; 2 Kor 8:1; 9:2,12 maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kutoa mchango kwa ajili ya watakatifu walio maskini huko Yerusalemu.

271 Kor 9:11; Rum 9:4 Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumia kwa mambo yao ya mwili.

28Basi nikiisha kuimaliza kazi hiyo, na kuwatilia mhuri tunda hilo, nitapitia kwenu, kwenda Spania.

29Rum 1:11 Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa baraka ya Kristo.

30 2 Kor 1:11; Flp 1:27; Kol 4:3; 2 The 3:1 Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;

31kwamba niokolewe kutoka kwa wale wasioamini katika Yudea, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu;

32nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi.

33Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help