Matendo 23 - Swahili Revised Union Version

1

22Basi yule jemadari akamwacha kijana aende zake, akimwagiza, Usimwambie mtu awaye yote ya kwamba umeniambia haya.

Paulo atumwa kwa Feliki mtawala

23Akawaita maofisa wawili, akasema, Wekeni tayari askari mia mbili kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, kabla ya saa tatu usiku.

24Akawaambia kuweka wanyama tayari wampandishe Paulo, na kumchukua salama kwa Feliki mtawala.

25Akaandika barua, juu ya hili,

26Lk 1:3 Klaudio Lisia kwa mtawala mtukufu Feliki, Salamu!

27Mdo 21:33; 22:25 Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi, wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni Mrumi.

28Mdo 22:30 Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamteremsha nikamweka mbele ya baraza;

29Mdo 6:9; 18:14,15 nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.

30Mdo 24:8 Hata nilipopewa habari kwamba patakuwa na ghasia juu ya mtu huyu, mara nikamtuma kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu.

31Basi, wale askari wakamchukua Paulo kama walivyoamriwa, wakampeleka hadi Antipatri usiku;

32hata asubuhi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja naye, nao wakarudi zao ngomeni.

33Na wale walipofika Kaisaria, na kumpa mtawala ile barua, wakamweka Paulo mbele yake.

34Mdo 22:3 Naye alipokwisha kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa mkoa gani? Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia,

35akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help