Mathayo 11 - Swahili Revised Union Version

Wajumbe kutoka kwa Yohana Mbatizaji

1 Mt 7:28; 13:53; 19:1; 26:1 Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

2 Lk 7:18-35 Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,Mt 14:3

3Mal 3:1; Dan 9:26 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumngojee mwingine?

4Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;

5Isa 35:5-6; 61:1 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.

6Mt 13:57; 26:31 Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.

Yesu amsifu Yohana Mbatizaji

7 Mt 3:1,5 Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?

8Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme.

9Lk 1:76 Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii.

10Mal 3:1; Mk 1:2; Yn 3:28 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,

Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu

Mbele ya uso wako,

Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.

11 Mt 13:17 Lakini, nawaambieni, Hajatokea mtu katika wazawa wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.

12Lk 16:16; 13:24; Yn 6:15 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu huuteka.

13Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.

14Mal 4:5; Mt 17:10-13; Mk 9:11-13 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.

15Mwenye masikio, na asikie.

16Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,

17Mit 29:9 Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.

18Mt 3:4 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Ana pepo.

19Mt 9:14,15 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

Ole Miji isiyotubu

20 Lk 10:12-15 Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.

21Isa 23:1-18; Eze 26:1—28:26; Yoe 3:4-8; Amo 1:9-10; Zek 9:2-4; Yon 3:6 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.

22Lakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.

23Isa 14:13-15; Mwa 19:24-28; Mt 4:13; 8:5; 9:1 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.

24Mt 10:15; Lk 10:12 Lakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe.

Yesu amshukuru Baba yake

25 Lk 10:21,22 Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.1 Kor 1:26-29

26Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.

27Yn 3:35; 1:18; 10:15; Mt 28:18; Flp 2:9 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

28Mt 12:20; Yer 31:25 Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29Yer 6:16 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

301 Yoh 5:3 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help