1
Na kilele cha Karmeli kitanyauka.
3 Isa 8:4; 2 Fal 10:33; 17:1-3; Yer 49:23-27; Zek 9:1 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma;
4lakini nitatuma moto uingie katika nyumba ya Hazaeli, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.
5Isa 7:1 Nami nitalivunja komeo la Dameski, na kuwakatilia mbali wenyeji wa bondeni mwa Aveni, na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Beth-Adini; na watu wa Shamu watakwenda uhamishoni hadi Kiri, asema BWANA.
6 2 Nya 28:18; Isa 14:29-31; Yer 47:1-7; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waiiteka nyara kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;
72 Fal 18:8 lakini nitatuma moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.
8Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.
9 Isa 23:1-18; Eze 26:1—28:19; Yoe 3:4-8; Zek 9:1-4; Mt 11:21-22; Lk 10:13-14 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;
10lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Tiro, nao utayateketeza majumba yake.
11 2 Nya 28:17; Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Oba 1-14; Mal 1:2-5 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararuararua daima, akaishika ghadhabu yake milele;
12lakini nitatuma moto juu ya Temani, nao utayateketeza majumba ya Bosra.
13 Yer 49:1-6; Eze 21:28-32; 25:1-7; Sef 2:8-11 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;
14Kum 3:11; Eze 25:5 lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela;
15Yer 49:3 na mfalme wao atakwenda utumwani, yeye na wakuu wake wote pamoja, asema BWANA.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.