1 wangu,
Wala msiwadhuru nabii zangu.
23 Zab 47:1; 96:1 Mwimbieni BWANA, nchi yote;
Tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
24 Isa 12:4 Watangazieni mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
25 Zab 24:8; 89:6-8; Isa 40:25,26 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26 Law 19:4; Zab 115:4-8; Isa 45:20; Yer 10:3; 1 Kor 8:4 Maana miungu yote ya watu si kitu;
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
27 Zab 8:1 Heshima na adhama ziko mbele zake;
Nguvu na furaha zipo mahali pake.
28Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
29Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Leteni sadaka, na mje mbele zake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
30Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
31 Isa 35:10; Lk 2:13; Ufu 14:2 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie;
Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;
32 Zab 96:10 Bahari na ivume na vyote viijazavyo;
Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
33Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,
Mbele za BWANA,
Kwa maana anakuja kuihukumu nchi.
34 Zab 106:1; 107:1; 118:1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
35 Zab 106:47,48 Nanyi semeni,
Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe,
Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
Tulishukuru jina lako takatifu,
Tuzifanyie shangwe sifa zako.
36 1 Fal 8:15; Zab 72:18,19; Kum 27:15; Neh 8:6 Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.
Ibada zarejeshwa tena37Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la Agano la BWANA, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake.
38Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu;
391 Nya 21:29; 2 Nya 1:3; 1 Fal 3:4 na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya BWANA katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni,
40Kut 29:38; Hes 28:3 ili kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, kulingana na yote yaliyoandikwa katika Torati ya BWANA, aliyowaamuru Israeli;
412 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Neh 9:17; Zab 25:10; 33:5; 100:5; Yer 33:11; Yoe 2:13; Lk 6:36; Yak 5:11 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;
42na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni.
432 Sam 6:19,20; Mwa 18:19; Yos 24:15 Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.