1 Mwa 4:25; 5:3,9 Adamu, na Sethi, na Enoshi;
2na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi;
3Yud 1:14 na Henoko, na Methusela, na Lameki;
4na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
5 Mwa 10:2 Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
6Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
7Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.
8 Mwa 16:0 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
9Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.
10Mwa 10:8,13 Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
11Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
12Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.
13Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
14na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;
15na Mhivi, na Mwarki, na Msini;
16na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17 Mwa 9:23,26; 10:22; 11:10 Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
18Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi.
19Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani.
20Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera;
21na Hadoramu, na Uzali, na Dikla;
22na Obali, na Abimaeli, na Sheba;
23na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24 Mwa 11:10; Lk 3:36 Shemu, na Arfaksadi, na Sala;
25Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35 na Eberi, na Pelegi, na Reu;
26na Serugi, na Nahori, na Tera;
27Mwa 17:5; 2 Nya 20:7; Neh 9:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16; Yak 2:23 na Abramu, naye ndiye Abrahamu.
Toka Abrahamu hadi Yakobo28 Mwa 21:2,3; 16:11,15 Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli.
29 Mwa 25:13-16 Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu;
30Mwa 25:15 na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;
31na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32 Mwa 25:1,2 Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
33Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34 Mwa 21:2,3; 25:25 Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.
35 Mwa 36:9,10; Kum 2:22; Mal 1:2,3; Rum 9:13; Ebr 12:16 Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.
36Mwa 36:11 Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.
37Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.
38Mwa 36:20 Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.
39Mwa 36:22 Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani.
40Mwa 36:23 Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.
41Mwa 36:25,26 Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
42Mwa 36:27 Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.
43 Mwa 36:31; 49:10 Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.
44Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake.
45Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake.
461 Fal 11:14 Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi.
47Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake.
48Mwa 36:37 Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake.
49Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake.
50Mwa 36:39 Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.
51Mwa 36:40; Kut 15:15 Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi;
52na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni;
53na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari;
54na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.