Isaya 21 - Swahili Revised Union Version

Utabiri juu ya Babeli, Edomu na Arabuni

1 zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka kwa nyika, toka nchi itishayo.

21 Sam 24:13; Yer 49:34; Isa 24:16; 13:17 Nimeoneshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote.

3Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, uchungu umenishika, kama uchungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona.

4Kum 28:67 Moyo wangu unapigapiga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha.

5Dan 5:5 Wanaandaa meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta.

6Maana Bwana ameniambia hivi, Nenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze.

7Naye akiona kundi la wapanda farasi, wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia; na asikilize kwa makini, kwa makini sana.

8Hab 2:1 Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu.

9Isa 13:19; Yer 50:2; Ufu 14:8; 18:2 Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini.

10Yer 51:33; Mik 4:13; Hab 3:12 Ewe wangu niliyekufikicha na kukupura; Hayo niliyoyasikia kwa BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, nayatangaza kwenu.

11 1 Nya 1:30; Eze 35:2; Oba 1:1 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?

12Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.

13 1 Nya 1:9 Ufunuo juu ya Arabuni.

Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala,

Enyi misafara ya Wadedani.

14 Ayu 6:19 Waleteeni wenye kiu maji,

Enyi wenyeji wa nchi ya Tema;

Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.

15Kwa maana wanakimbia mbele ya panga,

Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa,

Na mbele ya ukali wa vita.

16 Mwa 25:13; Zab 120:5; Wim 1:5; Isa 60:7 Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari.

17Hes 23:19; 1 Sam 15:29; Isa 1:20; Mt 24:35; Mk 13:31; Lk 21:33; 1 Pet 1:25 Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana BWANA, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help