1 Mt 21:33-46; Lk 20:9-19 Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.Isa 5:1-2
2Na kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu.
3Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, bila chochote.
4Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia majeraha ya kichwa, wakamfanyia jeuri.
5Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua.
6Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.
7Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu.
8Ebr 13:12 Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu.
9Basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.
10Zab 118:22-23 Hata andiko hili hamjalisoma,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
11Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu?
12Nao wakataka kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao.
Swali juu ya kulipa kodi13 Mt 22:15-22; Lk 20:20-26 Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno.Mk 3:6
14Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?
15Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.
16Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.
17Rum 13:7 Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.
Swali juu ya kufufuka18 Mdo 23:8; Mt 22:23-33; Lk 20:27-38 Kisha Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza na kusema,
19Kum 25:5,6; Mwa 38:8 Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.
20Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzawa.
21Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzawa. Na wa tatu kadhalika;
22hata na wote saba, wasiache mzawa. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
23Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.
24Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?
25Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.
26Kut 3:2,6; Mt 8:11; Lk 16:22 Na kuhusu wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Kuhusu kile kichaka jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?
27Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.
Amri ya kwanza28 Lk 10:25-28; Mt 22:34-40; Lk 20:39,40 Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?Lk 10:25-28
29Kum 6:4-5 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30Yn 15:12 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
31Law 19:18 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
32Kum 4:35; 6:4 Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;
33Hos 6:6; 1 Sam 15:22 na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhabihu zote pia.
34Mdo 26:27-29 Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumwuliza swali tena tokea hapo.
Swali juu ya Mwana wa Daudi35 Mt 22:41-46; Lk 20:41-44 Yesu alipokuwa akifundisha katika hekalu, alijibu, akasema, Husemaje waandishi ya kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi?
36Zab 110:1; 2 Sam 23:2; Yn 7:42 Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu,
Bwana alimwambia Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kulia,
Hata niwawekapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.
37Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na watu wengi walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.
Yesu awashutumu waandishi38 Mt 23:1-39; Lk 20:45-47 Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,
39na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele katika karamu;
40ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa.
Sadaka ya mjane41 Lk 21:1-4 Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.2 Fal 12:9
42Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
43Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
442 Kor 8:12 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.