1Kuhani Mkuu akasema, Je! Mambo hayo ndivyo yalivyo?
2Mwa 12:1; Zab 29:3; Mwa 11:31; 15:7 Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani,
3Mwa 12:1; 48:4 akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonesha.
4Mwa 11:31; 12:4 Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii mnayokaa ninyi sasa.
5Mwa 12:7; 13:15; 15:18; 17:8; 48:4; Kum 2:5 Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.
6Mwa 15:13-14; Kut 2:22; 12:40 Mungu akanena hivi, ya kwamba wazawa wake watakuwa wageni katika nchi ya watu wengine, nao watawafanya kuwa watumwa wao, na kuwatenda mabaya kwa muda wa miaka mia nne.
7Kut 3:12 Na lile taifa watakaowafanya watumwa nitawahukumu mimi, alisema Mungu; na baada ya hayo watatoka, nao wataniabudu mahali hapa.
8Mwa 17:10-14; 21:2-4; 25:26; 29:31—35:18 Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.
9 Mwa 37:11,28; 39:2,21; 45:4 Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja naye,
10Mwa 41:39-41; 39:21; Zab 105:21 akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.
11Mwa 42:1-2; 41:54 Basi kukawa na njaa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, na dhiki nyingi, wala baba zetu hawakupata chakula cha kuwatosha.
12Mwa 42:2 Hata Yakobo aliposikia ya kwamba huko Misri kuna nafaka, akawatuma baba zetu mara ya kwanza.
13Mwa 45:1,3,16 Hata safari ya pili Yusufu akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusufu ikawa dhahiri kwa Farao.
14Mwa 45:9-10; 17:18; Mwa 46:27; Kut 1:5; Kum 10:22 Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano.
15Mwa 46:1-7; 49:33; Kut 1:6 Basi Yakobo akashuka mpaka Misri; akafa yeye na baba zetu;
16Mwa 23:3-16; 33:19; 50:7-13; Yos 24:32 wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Abrahamu alilinunua kwa kima fulani cha fedha kutoka kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.
17 Kut 1:7-8 Basi wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimpa Abrahamu ulipokuwa unakaribia, wale watu wakazidi na kuongezeka sana huko Misri,
18hata mfalme mwingine asiyemfahamu Yusufu akaanza kutawala katika Misri.
19Kut 1:10-11,22; Mwa 24:7 Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi.
20Kut 2:2; Ebr 11:23 Wakati huo akazaliwa Musa, naye alikuwa mzuri sana, akalelewa muda wa miezi mitatu katika nyumba ya babaye.
21Kut 2:3-10 Wakati alipotupwa, binti Farao akamtwaa, akamlea awe kama mwanawe.
22Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.
23Kut 2:11-15 Umri wake ulipokuwa kama miaka arubaini akaazimu moyoni mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli.
24Kut 2:12 Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipizia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri.
25Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu.
26Kut 2:13 Kesho yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana?
27Kut 2:14; Lk 12:14 Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu?
28Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri jana?
29Kut 2:15,22; 18:3-4 Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa kama mgeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko.
30Kut 3:1-10; Kum 33:16 Hata miaka arubaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima wa Sinai katika muali wa moto, kichakani.
31Musa alipouona, akastaajabia maono yale, na alipokaribia ili atazame, sauti ya Bwana ikamjia,
32Kut 3:6 Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akatetemeka, asithubutu kutazama.
33Kut 3:5 Bwana akamwambia, Vua viatu miguuni mwako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu.
34Kut 2:24; 3:7,10 Hakika nimeona mateso ya watu wangu waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka niwatoe. Basi sasa, nitakutuma mpaka Misri.
35Kut 2:14 Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka.
36Kut 7:3,10; 14:21; Hes 14:33 Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arubaini.
37Kum 18:15,18; Mdo 3:22 Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye.
38Kut 19:1—20:17; Kum 5:1-33; Mdo 7:53; Kum 9:10 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima ili atupe sisi.
39Hes 14:3 Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarejea Misri,
40Kut 32:1,23 wakamwambia Haruni, Tutengenezee miungu, watakaotutangulia; maana huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui lililompata.
41Kut 32:2-6 Wakatengeneza ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao.
42Amo 5:25-27; Yer 19:13 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii,
Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka
Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
43Nanyi mlichukua hema ya Moleki,
Na nyota za mungu wenu Refani,
Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu;
Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
44 Kut 25:9,40 Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye kulingana na mfano ule aliouona;
45Yos 3:14-17; 18:1; Mwa 17:8; 48:4; Kum 32:49 ambayo baba zetu, kwa kupokezana, wakaiingiza pamoja na Yoshua katika milki ya Mataifa wale, ambao Mungu aliwafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daudi;
462 Sam 7:1-16; 1 Nya 17:1-14; Zab 132:5 aliyepata fadhili mbele za Mungu, naye aliomba ampatie Mungu wa Yakobo maskani.
471 Fal 6:1-38; 2 Nya 3:1-17 Lakini Sulemani alimjengea nyumba.
48Isa 66:1,2 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizojengwa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,
49 Isa 66:1-2 Mbingu ni kiti changu cha enzi,
Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu;
Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana,
50Au ni mahali gani nitakapostarehe?
Si mkono wangu uliofanya haya yote?
51 Isa 63:10; Kut 32:9; Law 26:41; Hes 27:14; Yer 9:26 Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo.
522 Nya 36:16; Mt 23:31 Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua;
53Kut 20:1-26; Gal 3:19; Ebr 2:2 ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika msiishike.
Kupigwa mawe kwa Stefano54 Mdo 5:33 Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno.
55Lk 22:69 Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kulia wa Mungu.
56Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kulia wa Mungu.
57Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja,
58Mdo 22:20 wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli.
59Zab 31:5; Lk 23:46 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.
60Lk 23:34 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.