Yuda UTANGULIZI - Swahili, Common Language Bible with DCs

UTANGULIZIBarua hii ya Yuda imeandikwa sio kwa jumuiya fulani ya kanisa, bali kwa jumuiya yote ya Kikristo. Mwandishi anajitaja kama “Yuda, nduguye Yakobo”. Katika Injili ya Marko hao wawili, Yuda na Yakobo, wanasemekana kuwa “nduguze Yesu”. Tunajua mengi juu ya Yakobo, kwamba yeye alikuwa na nafasi muhimu ya uongozi wa jumuiya ya waumini wa Kanisa la Yerusalemu, na pia mwandishi wa barua inayotajwa kwa jina lake. Lakini hatujui mengine juu ya Yuda.Mwandishi anatuambia kwamba alikuwa na lengo lake la kuandika juu ya msingi wa imani, lakini akalazimika kubadili na kuandika barua hii ya kuwashutumu waenezi wa mafundisho ya uongo ambao walijipenyeza kwa siri katika jumuiya ya waumini (3-16). Mwandishi anawaonya waumini wadumu imara katika imani (17-23) na kumalizia kwa utenzi wa sifa “kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote, sasa na hata milele! Amina” (24-25).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help