1Natazama juu milimani;
msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu,
aliyeumba mbingu na dunia.
3Hatakuacha uanguke;
mlinzi wako hasinzii.
4Kweli mlinzi wa Israeli
hasinzii wala halali.
5Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako;
yuko upande wako wa kulia kukukinga.
6Mchana jua halitakuumiza,
wala mwezi wakati wa usiku.
7Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote;
atayalinda salama maisha yako.
8Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote
tangu sasa na hata milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.