Zaburi 131 - Swahili, Common Language Bible with DCs

Kumtumainia Mungu kwa utulivu(Wimbo wa Kwenda Juu, wa Daudi)

1Ee Mwenyezi-Mungu, sina moyo wa kiburi;

mimi si mtu wa majivuno.

Sijishughulishi na mambo makuu,

au yaliyo ya ajabu mno kwangu.

2Ila nafsi yangu imetulia na kuwa na amani,

kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake;

ndivyo nafsi yangu ilivyo tulivu.

3Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu,

tangu sasa na hata milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help