Ezekieli 2 - Swahili, Common Language Bible with DCs

Ezekieli anaitwa kuwa nabii

1Naye akaniambia, “Wewe mtu! Simama wima. Nataka kuongea nawe.”

2Alipokuwa akiongea nami, roho ya Mungu ikaniingia na kunisimamisha wima. Ndipo nikamsikia

3akiniambia, “Wewe mtu nakutuma kwa Waisraeli, taifa la waasi ambao wameniasi. Wameendelea kunikosea mimi hadi leo kama walivyokuwa wazee wao.

4Watu hao ni wafidhuli na wajeuri. Nakutuma kwao, nawe utawaambia kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi na hivi.

5Wakisikia au wasiposikia, maana wao ni watu waasi, walau watatambua kwamba nabii amekuwapo miongoni mwao.

6Lakini, ewe mtu usiwaogope hao wala maneno yao. Hata kama mbigili na miiba vinakuzunguka, au unaketi juu ya nge, usiogope maneno yao wala usitishwe na nyuso zao, kwani hao ni watu waasi.

7Wewe utawaambia maneno yangu, hata kama watasikia au hawatasikia, maana wao ni watu waasi.

8“Lakini ewe mtu, sikiliza ninayokuambia, wala usiwe mwasi kama watu hao. Fumbua kinywa chako, ule ninachokupa.”

9 2:9-10 Taz Ufu 5:1 Nilipotazama, niliona nimenyoshewa mkono, na kumbe ulikuwa na kitabu kilichoandikwa.

10Basi akakifungua mbele yangu, nacho kilikuwa kimeandikwa mbele na nyuma maneno ya maombolezo, vilio na laana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help