Wimbo Ulio Bora 3 - Swahili, Common Language Bible with DCs

1Usiku nikiwa kitandani mwangu,

niliota namtafuta nimpendaye moyoni mwangu;

nilimtafuta, lakini sikumpata.

2Niliamka nikazunguka mjini,

barabarani na hata vichochoroni,

nikimtafuta yule wangu wa moyo.

Nilimtafuta, lakini sikumpata.

3Walinzi wa mji waliniona

walipokuwa wanazunguka mjini.

Basi nikawauliza,

“Je, mmemwona mpenzi wangu wa moyo?”

4Mara tu nilipoachana nao,

nilimwona mpenzi wangu wa moyo;

nikamshika wala sikumwachia aondoke,

hadi nilipompeleka nyumbani kwa mama yangu,

hadi chumbani kwake yule aliyenizaa.

5Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu,

kama walivyo paa au swala,

msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,

hadi hapo wakati wake utakapofika.

Shairi la tatuBibi arusi

6Ni kitu gani kile kitokacho jangwani

kama mnara wa moshi,

kinukiacho manemane na ubani,

manukato yauzwayo na wafanyabiashara?

7Tazama! Ni machela ya Solomoni;

amebebwa juu ya kiti chake cha enzi;

amezungukwa na walinzi sitini,

mashujaa bora wa Israeli.

8Kila mmoja wao ameshika upanga,

kila mmoja wao ni hodari wa vita.

Kila mmoja ana upanga wake mkononi,

tayari kumkabili adui usiku.

9Mfalme Solomoni alijitengenezea machela,

kwa mbao nzuri kutoka Lebanoni.

10Nguzo zake zilitengenezwa kwa fedha;

mgongo wake kwa dhahabu;

mahali pa kukalia pamefunikwa vitambaa vya zambarau,

walichoshona kwa upendo wanawake wa Yerusalemu,

waliokishonea alama za upendo.

11Njoni basi enyi wanawake wa Siyoni,

mkamwone mfalme Solomoni.

Amevalia taji aliyovikwa na mama yake,

siku alipofanya harusi yake,

naam, siku ambayo moyo wake ulijaa furaha.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help