Zaburi 45 - Swahili, Common Language Bible with DCs

Utenzi wa kumsifu mfalme(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Yungiyungi. Utenzi wa Wakorahi; utenzi wa mapenzi)

1Moyo wangu umejaa mawazo mema:

Namtungia mfalme shairi langu,

ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.

2Wewe u mzuri kuliko wanadamu wote,

maneno yako ni fadhili tupu.

Kwa hiyo Mungu amekubariki milele.

3Jifunge upanga wako, ewe shujaa!

Wewe ni mtukufu na mwenye fahari.

4Songa mbele kwa utukufu upate ushindi,

utetee ukweli na kulinda haki.

Mkono wako utende mambo makuu.

5Mishale yako ni mikali,

hupenya mioyo ya maadui za mfalme;

nayo mataifa huanguka chini yako.

6

chadumu milele kama cha Mungu.

Wewe watawala watu wako kwa haki.

7Wapenda uadilifu na kuchukia uovu.

Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuteua,

na kukupa furaha kuliko wenzako.

8Mavazi yako yanukia marashi na udi,

wanamuziki wakuimbia katika majumba ya pembe za ndovu.

9Binti za wafalme ni baadhi ya wanaokulaki,

naye malkia amesimama kulia kwako,

amevaa mapambo ya dhahabu safi ya Ofiri.

10Sikiliza binti, ufikirie!

Tega sikio lako:

Sahau sasa watu wako na jamaa zako.

11Uzuri wako wamvutia mfalme;

yeye ni bwana wako, lazima umtii.

12Watu wa Tiro watakuletea zawadi;

matajiri watataka upendeleo wako.

13Binti mfalme anaingia mzuri kabisa!

Vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.

14Akiwa amevalia vazi la rangi nyingi,

anaongozwa kwa mfalme,

akisindikizwa na wasichana wenzake;

nao pia wanapelekwa kwa mfalme.

15Kwa furaha na shangwe wanafika huko,

na kuingia katika jumba la mfalme.

16Ee mfalme, utapata watoto wengi

watakaotawala mahali pa wazee wako;

utawafanya watawale duniani kote.

17Nitalifanya jina lako litukuzwe katika vizazi vyote,

nayo mataifa yatakusifu daima na milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help