Yudithi UTANGULIZI - Swahili, Common Language Bible with DCs

UTANGULIZIKitabu cha Yudithi ni simulizi la ushindi walioupata watu wateule wa Mungu dhidi ya maadui zao kwa bidii na ujasiri wa mwanamke. Jumuiya ndogo ya Wayahudi inakabiliana na hali mbaya ambayo jeshi la Holoferne linakusudia kuuweka ulimwengu wote chini ya mamlaka ya Nebukadneza na kuangamiza dini zozote zile isipokuwa ile ya Nebukadneza ambaye kwa kweli amefanywa kuwa mungu. Hapo ndipo anapoingia Yudithi. Anawalaumu viongozi wa miji kwa utovu wao wa imani kwa Mungu.Simulizi lenyewe halijali sana hali kamili ya kihistoria wala jiografia, hata Nebukadneza anatajwa hapa kama mfalme wa Ashuru! Tena matukio haya yanaonesha kwamba Wayahudi walikwisha rudi kutoka uhamishoni (4:3; 5:11); hali Nebukadneza ndiye mwenyewe aliyewachukua uhamishoni.Shabaha ya kitabu hiki ni kuwatia moyo wananchi wenzake Yudithi wanapokabiliana na hali ngumu na kuwahimiza hasa wabaki waaminifu kwa Mungu katika hali yoyote ile. Kitabu chenyewe basi chafanana kuhusu malengo hayo na kitabu cha Danieli.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help