1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,
2 kwa Mwenyezi-Mungu.
25Lakini matunda ya kuanzia mwaka wa tano hayo mnaweza kula, na mavuno yenu yataongezeka. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
26 Taz Mwa 9:4; Lawi 7:26-27; 17:10-14; Kumb 12:16,23; 15:23; 18:10 “Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi.
27Taz Lawi 2:5; Kumb 14;1 Nywele zenu msizikate pembeni wala kunyoa ndevu zenu.
28Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
29 Taz Kumb 23:17 “Usimchafue binti yako kwa kumfanya kahaba, nchi nzima isije ikaangukia katika ukahaba na hivyo kujaa uovu.
30Taz Lawi 26:2 Mtazishika Sabato zangu na kupaheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
31 Taz Kumb 18:11; 1Sam 28:3; 2Fal 23:4; Isa 8:19 “Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
32“Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
33“Kama kuna mgeni katika nchi yako usimtendee vibaya.
34Huyo mgeni anayekaa nawe atakuwa kwako kama mwenyeji nawe utampenda kama unavyojipenda mwenyewe, kwa kuwa nawe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
35 Taz Kut 22:21; Kumb 24:14-18; 27:19 “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo.
36Ni lazima mtumie mizani halali, na vipimo vilivyo halali. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri.
37Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.