Zekaria UTANGULIZI - Swahili, Common Language Bible with DCs

UTANGULIZIKitabu cha Zekaria chaweza kuitwa kitabu cha matumaini. Kitabu chenyewe kina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza (sura 1–8) ina mahubiri ya nabii yaliyotolewa kati ya mwaka 520 na 518 K. K. Mahubiri hayo ya kinabii mara nyingi yanafanyika kwa njia ya maono, na yanasisitiza kwamba ujenzi mpya wa hekalu na kurekebishwa mji wa Yerusalemu kutakuwa alama au ishara ya kuwasili nyakati mpya za nafuu. Nyakati hizo zitaanzishwa na Mungu kwa kumteua mtawala Zerubabeli na kuhani mkuu Yoshua. Tumaini la Waisraeli linaelekezwa juu ya kungojea kwa hamu wakati ule Mungu atakapotawala juu ya nchi yote.Sehemu ya pili ya kitabu hiki (sura 9–14) inasisitiza juu ya mambo mawili: La kwanza ni juu ya hali na tabia maalumu za huyo mtu atakayetumiwa na Mungu kuanzisha utawala wa Mungu. Huyo anaelezwa kama mfalme mnyenyekevu na mwenye ushindi; mfalme aliye kama kondoo anayepelekwa kuuawa. Katika Agano Jipya waandishi wa Injili wanadokeza mtazamo huo kueleza utumishi wa Yesu hasa kuhusu kifo chake (taz Mat 21:4-5; 26:31; Marko 14:27 na Yoh 19:37).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help