Zaburi 28 - Swahili, Common Language Bible with DCs

Kuomba msaada(Zaburi ya Daudi)

1Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu!

Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi,

la sivyo kama usiponisikiliza,

nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu.

2Sikiliza sauti ya ombi langu,

ninapokulilia unisaidie,

ninapoinua mikono yangu kuelekea maskani yako takatifu.

3Usinipatilize pamoja na watu wabaya,

pamoja na watu watendao maovu:

Watu wasemao na wenzao maneno ya amani,

kumbe wamejaa uhasama moyoni.

4 Taz Ufu 22:12 Uwaadhibu kadiri ya matendo yao,

kufuatana na maovu waliyotenda.

Waadhibu kadiri ya matendo yao wenyewe;

uwatendee yale wanayostahili.

5Hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu;

hawatambui mambo aliyoyafanya.

Kwa sababu hiyo atawabomoa,

wala hatawajenga tena upya.

6Atukuzwe Mwenyezi-Mungu,

maana amesikiliza ombi langu.

7Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu;

tegemeo la moyo wangu limo kwake.

Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo;

kwa wimbo wangu ninamshukuru.

8Mwenyezi-Mungu ni nguvu ya watu wake;

yeye ni kimbilio la wokovu kwa mfalme wake mteule.

9Ee Mungu, uwaokoe watu wako;

uwabariki watu hao walio mali yako.

Uwe mchungaji wao na kuwategemeza milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help