Zaburi 26 - Swahili, Common Language Bible with DCs

Sala ya mtu mwema(Zaburi ya Daudi)

1Ee Mwenyezi-Mungu, unitetee,

maana nimeishi bila hatia,

nimekutumainia wewe bila kusita.

2Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima;

uchunguze moyo wangu na akili zangu.

3Fadhili zako ziko mbele ya macho yangu,

ninaishi kutokana na uaminifu wako.

4Sijumuiki na watu wapotovu;

sishirikiani na watu wanafiki.

5Nachukia mikutano ya wabaya;

wala sitajumuika na waovu.

6Nanawa mikono yangu kuonesha sina hatia,

na kuizunguka madhabahu yako, ee Mwenyezi-Mungu,

7nikiimba wimbo wa shukrani,

na kusimulia matendo yako yote ya ajabu.

8Ee Mwenyezi-Mungu, napenda makao yako,

mahali unapokaa utukufu wako.

9Usiniangamize pamoja na wenye dhambi,

wala usinitupe pamoja na wauaji,

10watu ambao matendo yao ni maovu daima,

watu ambao wamejaa rushwa.

11Lakini mimi ninaishi kwa unyofu;

unihurumie na kunikomboa.

12Mimi nimesimama mahali palipo imara;

nitamsifu Mwenyezi-Mungu katika kusanyiko kubwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help