Waebrania 1 - Kiswahili Study Bible

Mungu anasema kwa njia ya Mwanae

1Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,

2lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu, akamteua avimiliki vitu vyote.

3Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwatakasa binadamu dhambi zao, ameketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.Ukuu wa Mwana wa Mungu

4Mwana ni mkuu kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu kuliko jina lao.

5Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:

“Wewe ni Mwanangu;

mimi leo nimekuwa Baba yako.”

Wala hakusema juu ya malaika yeyote:

“Mimi nitakuwa Baba yake,

naye atakuwa Mwanangu.”

6Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae, mzaliwa wa kwanza, ulimwenguni alisema:

“Malaika wote wa Mungu na wamwabudu.”

7Lakini kuhusu malaika, alisema:

“Amewafanya malaika wake kuwa upepo,

na wahudumu wake ndimi za moto.”

8Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema:

“Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumu milele na milele!

Wewe wawatawala watu wako kwa haki.

9Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu.

Ndiyo maana Mungu, Mungu wako, amekuweka wakfu

na kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako.”

10Na tena:

“Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo,

mbingu ni kazi ya mikono yako.

11Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima,

zote zitachakaa kama vazi.

12Utazikunjakunja kama koti,

nazo zitabadilishwa kama vazi.

Lakini wewe ni yuleyule daima,

na maisha yako hayatakoma.”

13Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake:

“Keti upande wangu wa kulia,

mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.”

14 na ambao hutumwa kuwasaidia wale watakaopokea wokovu?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help