Zaburi 54 - Kiswahili Study Bible

Sala ya kujikinga na maadui(Kwa Mwimbishaji: na ala za nyuzi za muziki. Utenzi wa Daudi wakati mtu mmoja kutoka Zifu alipomwendea Shauli na kumjulisha kuwa Daudi amejificha kwao.)

1Uniokoe, ee Mungu, kwa jina lako;

unitetee kwa nguvu yako.

2Uisikie, ee Mungu, sala yangu;

uyategee sikio maneno ya kinywa changu.

3Watu wenye kiburi wananishambulia;

wakatili wanayawinda maisha yangu,

watu ambao hawamjali Mungu.

4Najua Mungu ni msaada wangu,

Mwenyezi-Mungu hutegemeza maisha yangu.

5Yeye atawaadhibu maadui zangu kwa uovu wao wenyewe;

kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize.

6Nitakutolea tambiko kwa moyo mkunjufu;

nitakushukuru kwa kuwa ni vema.

7Maana umeniokoa katika taabu zangu zote,

nami nimewaona maadui zangu wameshindwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help