1 mwana wa Yairi, mwana wa Shemi, mwana wa Kishi kutoka katika kabila la Benyamini, aliota ndoto.
2Mordekai alikuwa Myahudi na aliishi katika mji mkuu wa Susa.
Yeye alikuwa mtu maarufu na mtumishi katika ikulu ya mfalme Ahasuero.3Mordekai alikuwa mmoja wa mateka ambao mfalme Nebukadneza
wa Babuloni aliwahamisha kutoka Yerusalemu akawapeleka hadi Babuloni pamoja na mfalme Yekonia wa Yudea.Ndoto aliyoota Mordekai ilikuwa hivi:
4Mordekai aliota kuna kelele, ghasia, ngurumo na mtetemeko wa ardhi,
pamoja na machafuko duniani.5Kisha kukatokea majoka
mawili makubwa yaliyokuwa tayari kupigana, nayo yalitoa mlio wa kutisha.6Kwa mlio wao huo mataifa yote yakajiandaa kupigana vita na watu wa Mungu, taifa adilifu.
7Siku hiyo ilikuwa ya giza na huzuni, majonzi na udhia, msiba na fujo duniani kote.
8Taifa lile lote adilifu lilisumbuliwa, likihofia maovu yatakayolikumba. Watu wakajiandaa kufa.
9Basi, wakamlilia Mungu, na kwa kilio chao, mto mkubwa uliotiririka maji mengi ukatokea kutoka kitu kilichoonekana kama kijito tu.
10Kulipopambazuka, jua lilichomoza, na wale wanyonge wakapata nguvu,
wakawaangamiza adui zao waheshimiwa.11Kwa ndoto hiyo, Mordekai aliona yale aliyodhamiria Mungu kuyafanya. Baada ya kuamka, alikuwa nayo akilini mwake na akatamani kujua kinaganaga maana ya ndoto hiyo siku nzima.
Mordekai ayaokoa maisha ya mfalme12 Mordekai alipokuwa akipumzika kwenye ua wa ikulu pamoja na Gabatha na Thara, matowashi wawili wa mfalme, walinzi wa uani,
13aliwasikia hao matowashi wakizungumza. Akasikiliza kwa makini kile walichokuwa wakizungumzia, kumbe, walikuwa wanakula njama kumuua mfalme. Basi, Mordekai akamwendea mfalme Ahasuero na kumweleza njama za matowashi hao wawili.
14Mfalme akaagiza wahojiwe, na walipokiri njama yao, wakatolewa nje na kunyongwa.
15 Mfalme aliamuru kumbukumbu juu ya tukio hilo iandikwe katika kitabu cha kumbukumbu za kifalme, naye Mordekai ndiye aliyeliandika.
16Kisha, mfalme akamweka Mordekai kuwa mhudumu kwenye ua na akampa zawadi kutokana na kuzifichua njama hizo.
17Lakini Hamani mwana wa Hamedatha, wa ukoo wa Bouga, mtu aliyeheshimiwa sana na mfalme, akaanza kutafuta njia ya kumdhuru Mordekai na Wayahudi wengine kwa sababu ndiye aliyehusika na vifo vya wale matowashi wawili wa mfalme.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.