1Mwenyezi-Mungu amwambia bwana wangu:
“Keti upande wangu wa kulia,
hata niwaweke maadui zako chini ya miguu yako.”
2Mwenyezi-Mungu ataeneza enzi yako kutoka Siyoni;
utatawala juu ya maadui zako wote.
3Watu wako watakujia kwa hiari,
siku utakapokwenda kuwapiga maadui.
Juu ya milima mitakatifu watakujia vijana wako,
kama umande unaotokeza alfajiri mapema.
4Mwenyezi-Mungu amekuapia wala hatabadili nia yake:
“Wewe ni kuhani milele kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.”
5Bwana yuko upande wako wa kulia;
atawaponda wafalme atakapokasirika.
6Atayahukumu mataifa na kuwaua watu wengi;
atawaponda viongozi kila mahali duniani.
7Mfalme atakunywa maji ya kijito njiani;
naye atainua kichwa juu kwa ushindi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.