Zaburi 70 - Kiswahili Study Bible

Kuomba msaada(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudiya matoleo ya ukumbusho)

1Upende kuniokoa ee Mungu!

Ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia.

2Wanaonuia kuniangamiza,

na waaibike na kufedheheka!

Hao wanaotamani niumie,

na warudi nyuma na kuaibika.

3Hao wanaonisimanga,

na wapumbazike kwa kushindwa kwao.

4Lakini wote wale wanaokutafuta,

wafurahi na kushangilia kwa sababu yako.

Wapendao wokovu wako,

waseme daima: “Mungu ni mkuu!”

5Nami niliye maskini na fukara,

unijie haraka, ee Mungu!

Ndiwe msaada wangu na mkombozi wangu;

ee Mwenyezi-Mungu, usikawie!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help