Zaburi 47 - Kiswahili Study Bible

Mungu, Mfalme wa ulimwengu wote(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Wakorahi)

1Enyi watu wote, pigeni makofi!

Msifuni Mungu kwa sauti za shangwe!

2Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, anatisha.

Yeye ni Mfalme mkuu wa ulimwengu wote.

3Ametuwezesha kuwashinda watu wa mataifa,

ameyaweka mataifa chini ya mamlaka yetu.

4Ametuchagulia nchi hii iwe urithi wetu,

ambayo ni fahari ya Yakobo anayempenda.

5Mungu amepanda juu na vigelegele,

Mwenyezi-Mungu na sauti ya tarumbeta.

6Mwimbieni Mungu sifa, mwimbieni!

Mwimbieni mfalme wetu sifa, mwimbieni!

7Mwimbieni Mungu sifa kwa tenzi;

maana yeye ni mfalme wa ulimwengu wote.

8Mungu anayatawala mataifa yote;

amekaa katika kiti chake cha enzi kitakatifu.

9Viongozi wa watu wa mataifa wanakusanyika,

wanajiunga na watu wa Mungu wa Abrahamu,

maana nguvu zote duniani ni zake Mungu,

yeye ametukuka sana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help