1Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,
kweli jina lako latukuka duniani kote!
Utukufu wako waenea mpaka juu ya mbingu!
2Kwa sifa za watoto wadogo na wanyonyao,
umejiwekea ngome dhidi ya adui zako,
uwakomeshe waasi na wapinzani wako.
3Nikiangalia mbingu, kazi ya vidole vyako,
mwezi na nyota ulizozisimika huko,
4mtu ni nini, ee Mungu, hata umfikirie,
binadamu ni nini hata umjali?
5Umemfanya awe karibu kama Mungu,
umemvika fahari na heshima.
6Ulimpa madaraka juu ya kazi zako zote;
uliviweka viumbe vyote chini ya mamlaka yake:
7kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini;
8ndege, samaki, na viumbe vyote vya baharini.
9Ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wetu,
kweli jina lako latukuka duniani kote!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.