3 Yohane UTANGULIZI - Swahili Common Language DC Bible

UTANGULIZIBarua hii ya tatu ya Yohane, kama ile ya pili, ni fupi sana. Hata hapa mwandishi anajitaja kama “Mzee” (taz 2 Yohane) na anayeandikiwa anatajwa kama Gayo ambaye ni rafiki wa pekee wa mwandishi. Hatujui chochote kuhusu huyu Gayo isipokuwa tu kwamba alikuwa mwaamini na alikuwa imara katika kumwamini Kristo. Habari tunayoambiwa juu yake ni kinyume kabisa cha habari za mtu mwingine anayetajwa katika barua hii yaani Diotrefe. Huyu bila shaka alikuwa mtu mashuhuri katika jumuiya ya Wakristo ambaye alimpuuza huyo “Mzee” na kukosa ukarimu.Mwandishi anamsifu Gayo kwa uaminifu na utumishi wake (taz 1-8); anashutumu mwenendo wa Diotrefe (taz 9-10), kisha anataja tabia njema ya mwaamini mwingine aitwaye Demetrio (11-12) na kumalizia kwa kuzungumzia ziara yake ya kulitembelea hilo kanisa, na mwishoni salamu za mwisho (12-15).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help