Yona UTANGULIZI - Swahili Common Language DC Bible
UTANGULIZITofauti sana na vitabu vingine vya manabii, kitabu cha Yona ni simulizi. Kinasimulia habari za nabii mmoja ambaye anatajwa mara moja tu katika A.K. katika (2 Fal 14:25). Yona anajaribu kwanza kukwepa wito wa Mungu na baadaye ananung'unika kwamba alipofuata wito huo wa kwenda kuhubiri, yalipatikana mafanikio ambayo hakuyatazamia. Waninewi walitubu, naye Yona hakupendezwa. Fundisho kubwa: Mungu mwenyewe anaongoza wasemaji wake bila ya wao kutaka. Pili: Binadamu hawezi kumwekea Mungu mipaka ya upendo wake kwa watu wake.