Isaya 17 - Swahili Common Language DC Bible

Mungu ataadhibu Ashuru na Israeli

1

Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”

Mwisho wa kuabudu sanamu

7Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli.

8Hawatazielekea tena madhabahu ambazo ni kazi za mikono yao wenyewe, wala kuzitazamia tena kazi za mikono yao wenyewe, yaani sanamu za mungu Ashera na madhabahu za kufukizia ubani.

9Siku hiyo miji yao imara itaachwa mahame, kama miji ambayo Wahivi na Waamori waliihama walipokuwa wakiwakimbia wazawa wa Israeli. Kila kitu kitakuwa uharibifu.

10Maana wewe Israeli umemsahau Mungu aliyekuokoa,

hukumkumbuka Mwamba wa usalama wako.

Kwa hiyo, hata mkipanda mimea ya Baali,

na kuiweka wakfu kwa mungu wa kigeni;

11hata mkiifanya ikue siku hiyohiyo mliyoipanda

na kuifanya ichanue asubuhi hiyohiyo,

mavuno yenu yatatoweka

siku hiyo ya balaa na maumivu yasiyoponyeka.

Mataifa adui yanashindwa

12Lo! Ngurumo ya watu wengi!

Wananguruma kama bahari.

Lo! Mlio wa watu wa mataifa!

Yanatoa mlio kama wa maji mengi.

13Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi,

lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali.

Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo;

kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.

14Wakati wa jioni yanaleta hofu kuu,

lakini kabla ya asubuhi yametoweka!

Hilo ndilo litakalowapata wanaonyakua mali yetu,

ndilo litakalowapata wanaotupora.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help