2 Yohane UTANGULIZI - Swahili Common Language DC Bible

UTANGULIZIMwandishi wa barua hii anajiita “Mzee” na ni dhahiri jina hili latumiwa kuonesha kwamba mwandishi aliheshimika katika jumuiya. Na anayeandikiwa anatajwa kama “Bimkubwa mteule, pamoja na watoto wako” maneno ambayo bila shaka yanatumika hapa kwa mfano wa jumuiya ya kanisa la mahali fulani (1:1).Barua yenyewe yawatia moyo wasomaji wake waishi kwa kuzingatia ukweli na upendo; hayo mawili yamaanisha kuwa waumini wanapaswa kushika amri za Mungu. Barua hii pia inawaonya wasomaji wake wawe na tahadhari juu ya mafundisho ya uongo, jambo ambalo lilitajwa pia katika barua ya kwanza. Na kama vile katika barua ile ya kwanza, mwandishi anawahimiza waumini wawe waangalifu na kudumu katika imani ya kweli.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help