Zaburi 84 - Swahili Common Language DC Bible

Hamu ya kuwa nyumbani kwa Mungu(Kwa Mwimbishaji: Mtindo wa Gitithi. Zaburi ya Wakorahi)

1Jinsi gani yanavyopendeza makao yako,

ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi!

2Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu!

Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai.

3Hata shomoro wamepata makao yao,

mbayuwayu wamejenga viota vyao,

humo wameweka makinda yao,

katika madhabahu zako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi,

Mfalme wangu na Mungu wangu!

4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,

wakiimba daima sifa zako.

5Heri watu wanaopata nguvu zao kwako,

wanaotamani kwenda kuhiji mlimani kwako.

6Wapitapo katika bonde kavu la Baka,

hulifanya kuwa mahali pa chemchemi,

na mvua za vuli hulijaza madimbwi.

7Wanaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi;

watamwona Mungu wa miungu huko Siyoni.

8Usikie sala yangu ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi;

unitegee sikio, ee Mungu wa Yakobo.

9Ee Mungu, umwangalie kwa wema ngao yetu mfalme,

umtazame huyo uliyemweka wakfu kwa mafuta.

10Siku moja tu katika maskani yako,

ni bora kuliko siku elfu mahali pengine;

afadhali kusimama mlangoni pa nyumba yako,

kuliko kuishi nyumbani kwa watu waovu.

11Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu;

yeye hutuneemesha na kutujalia fahari.

Hawanyimi chochote kilicho chema,

wale waishio kwa unyofu.

12Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi,

heri mtu yule anayekutumainia wewe!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help